Mshambulizi Michael Olunga Likizoni, Achambua Rosecoco

ByEdgar Wabwire
Published on: Jun 30, 2023 04:06
...
Michael Olunga Akisherekea baada ya kufunga bao. Picha Hisani

Mshambulizi matata na nahodha wa timu ya taifa Harambee stars Michael Olunga yuko nchini kwenye likizo ndefu baada ya msimu wa soka nchini Qatar kukamilika.

Mpachika magoli huyo wa zamani wa klabu ya Gor Mahia anayewajibikia timu ya Al Duhail amekuwa akiipigia debe timu yake ya kandanda ya MOA kwa sasa yuko kitongojini alikokopolewa akijivinjari.

Kupitia mtandao wake wa kijamii, Straika huyo alionekana ameketi chini huku akiwa ameshikilia uteo uliokuwa umesheheni maharage.

Olunga aliwachekesha baadhi ya mashabiki wake kwa kuandika kwamba alikuwa anafurahia kutenga maharage aina ya Rose coco kutoka kwa mpunga na uchafu mwingine, wengi wakisoma ujumbe tofauti na zoezi hilo kwani jina Rose Coco limekuwa likitumiwa kama istilahi kwenye miktadha mbalimbali.

“Fomu ni kuchambua rose coco. Ocha ndio best,” Olunga aliandika kwenye picha hiyo iliyomuonyesha anachambua maharage kwenye uteo. 

Mwanasoka huyo aliendelea kuchimbua na kuwazuzua wafuasi wake hata Zaidi kwa kuwauliza aina ya maharage wanayopenda kati ya rose coco na Njahi. 

“Rose Coco ndio best. Unapenda gani kati ya rose coco na Njahe?” aliuliza Olunga.

Baadhi ya mashabiki zake wakitoa hisia mseto kwa kuwa Jina Rose Coco alilotumia Olunga halikuwa lina sawiri maana ya kile walichokielewa mashabiki.

“mkuu rosecoco kwanza fresh from the garden” Aliandika Peter Opondo

“Rosecoco kwanza u mix na cucumber” Alisema Michael Ja Kusagi 


 


Leave a Comment..

0 Comments

No comments yet...